Christina akiwa nyumbani kwa mama Gladness Williamu alipo fika kuomba kazi                     


 Mapema leo katikati ya mji wa Mafinga wilayani Mufindi mkoani Iringa, mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 11 aliyejitambulisha kwa jina la Christina Kikoti ameonekana katika maeneo ya Pareto akizunguka majumbani kwa watu akiomba kazi.

Mtoto huyo ambaye kwamujibu wa akina mama waliompokea wamemkuta akiwa na majeraha ya kupigwa na kuumwa kwa meno mwilini huku akivuja damu kichwani na walipo taka kufahamu sababu mtoto ameeleza kupigwa na dada yake ambaye amekuwa akiishi naye.

Mtoto Christina ambaye ni yatima aliyewapoteza wazazi wote kwa sauti ya unyonge amezungumza na Chumba cha habari cha Ebony fm ambapo kwa mujibu wa maelezo yake amedai kuwa awali alikuwa akiishi na bibi yake katika kijiji cha Dabaga wilayani Kilolo.

Mtoto Christina aliyekuwa akisoma shule ya msingi alichululiwa na binamu yake kwenda kuishi Mjini mafinga ambapo amedai kuwa amekuwa akipigwa na dada yake huyo kisha kuamua kutafuta kazi ili kukwepa mateso hayo. 

Majirani waliojitokeza kumshuhudia mtoto huto na wamejaribu kutoa picha halisi ya muonekano wa mtoto huyo.

Mpaka sasa Ebony fm inafanya jitihada za kuwapata viongozi katika eneo hilo ili kufahamu jitihada za kumuhifadhi mtoto huyo.

 Mtoto Christina akiwa Nyumbani kwa mama aliyempokea Gladness William.

Jeraha la kichwani likivuja damu.

Post a Comment

 
Top