Oscar Pistorius amejitetea kwamba alimpiga risasi kimakosa mpenzi wake Reeva

Kiongozi wa mashtaka kwenye kesi ya mauaji inayomkabili mwanariadha mlemavu raia wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amemtaja mshtakiwa kama mtu aliyekolea uongO.

Kwenye taarifa yake ya mwisho kiongozi wa mshataka Gerrie Nel amesema kuwa Pistorius alimuua mpenziwe Reeva Steenkamp nyumbani kwake mjini Pretoria mwaka uliyopita.
Bwana Nel alikataa taarifa kutoka kwa upande unaomtetea Pistorius kuwa mwanariadha huyo alimuaa mpenziwe kimakosa akidhania kuwa alikuwa ni jambazi aliyengia nyumbani kwake.

Mamake Reeva akiwa Mahakamani

Wakili wa Pistorius naye alitoa taaraifa yake ya mwisho ambayo inatarajiwa kundelea pia kesho ijumaa akiwalaumu polisi kwa kuvuruga eneo kulikotokea mauaji.

Baadaye mahakama hiyo itatoa umauzi wake wa mwisho kuhusu hatma ya mwanariadha huyo.
Bwana Pistorius anatuhumiwa kwa mauaji ya mpenzi wake, Reeva Steenkamp, nyumbani kwake mjini Pretoria mwaka jana.

Wakili wa upande wa mashitaka Gerrie Nel amesema sio ukweli kuwa Pistorius alimpiga risasi mpenzi wake kimakosa akidhani kwamba alikuwa jambazi.

Mauaji hayo yalitokea tarehe 14 mwezi Februari mwaka jana.
Kiongozi wa mashitaka Gerrie Nel

Wakili wa Pistorius pia anatarajiwa kutoa kauli yake ya mwisho kuhusiana na kesi hiyo.
Kesi hiyo iliahirishwa mwezi jana kabla hatua hii ya pande zote kutoa kauli zao za mwisho na kesi kuamuliwa kufika.

Bwana Pistorius alisema alimpiga risasi Reeva kutokana na uoga kwani alidhani alikuwa mwizi aliyekuwa amevamia nyumba yake.

Hata hivyo wakili wa upinzani ameambia mahakama haipaswi kuwa a ugumu wowote katika kukataa ushahidi wa Pistorius kwa sababu hauna msingi na kwamba ni uongo.

Pia amesema Pistorius amejidai kuwa mwathiriwa kwa njia moja au nyingine kutokana na ulemavu wake.
Babake Pistorois ambaye hajakuwa maishani mwake kwa miaka mingi alikuwa mahakamani kwa mara ya kwanza tangu kesi hiyo kuanza kusikilizwa.

Babake marehemu Reeva pia alifika mahakamani kwa mara ya kwanza.
BBC-Swahili

Post a Comment

 
Top