Msanii wa muziki Recho almaarufu kama Recho Upepo ambaye alitamba na nyimbo kama Upepo, Kizunguzungu, amefunguka na kusema kuwa yeye hatumii madawa ya kulevya kama ambavyo watu mtaani wanavyodai.

 Msanii huyo ambaye sasa ameachia wimbo mpya unaoitwa 'Tour' amesema kuwa yeye hajui hata hiyo ladha ya unga ila anahisi ni kutokana na yeye kufananishwa na msanii mkongwe katika muziki Rehema Chalamila ambaye awali alikuwa akitumia madawa hayo ya kulevya.

"Kiukweli mimi situmii madawa ya kulevya hata kidogo, na huwa naumia sana roho napokuwa naambiwa hizi taarifa juu ya kutumia madawa ya kulevya, siijui hata ladha yake ila nadhani watu wanakuwa wakinifananisha, unajua mimi huwa nafananishwa sana na Ray C hivyo labda ndiyo sababu ya hizi taarifa kuwepo mtanii ila kiukweli mimi si mtumiaji wa madawa ya kulevya".

Lakini katika kumbukumbu msanii Recho alihusishwa kuwa na mahusiano na msanii TID na ndipo hapo watu walianza kudai kuwa amejifunza kutumia madawa ya kulevya alipoanzisha mahusiano na msanii huyo jambo ambalo yeye mwenyewe amelikana na kusema kuwa hatumii madawa ya kulevya aina yoyote ile na kusema anazushiwa tu hilo jambo, pia Recho alisema kuwa nje ya kazi yake ya muziki kwa sasa anafanya biashara ya urembo na vitu vya wanawake kama vipodozi kama njia ya kujiongezea kipato nje ya kazi yake hiyo ya muziki.

Awali msanii Recho alipoanza kutoka kisanii alikuwa akifananishwa na Ray C kutokana na wasanii hao kufanya vitu vilivyokuwa vikifanana kisanaa.

Katika hatua nyingine msanii huyo ameweka wazi na kumshukuru msanii wa Bongo Fleva Barnaba Boy kwa kuweza kumuandikia baadhi ya nyimbo toka anatoka na huu wimbo wake mpya Tour ambao amerekodi kwa producer Imma ze Boy.

Post a Comment

 
Top