Wagonjwa
wakimtia adabu Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Nyakabale mkoani
Geita, Josephat Msafiri baada ya kuwatelekeza juzi. Picha Jackline
Masinde.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Geita, Magreth Nakainga amemvua madaraka Mganga Mkuu wa Zahanati ya
Nyakabale, Josephat Msafiri kwa kukiuka miiko ya kazi yake na kulewa wakati wa
kazi.
Mkurugenzi huyo aliamua kuchukua uamuzi
huo jana kutokana na tukio lililotokea Juzi hii la daktari huyo kufunga kituo
cha afya na kuacha wagonjwa wakiwa wamezidiwa, kisha kwenda kunywa pombe jambo
lililowalazima kumchapa viboko akiwa baa.
“Tumeshamchukulia hatua za kinidhamu
ikiwa ni pamoja na kumvua madaraka yake ili iwe fundisho kwa watumishi wengine
wa Serikali,” alisema Nakainga.
Alisema kitendo alichokifanya
kimeidhalilisha taaluma ya afya na madaktari kwa ujumla.
Alisema tabia kama hizo hazitavumilika
kwa mtumishi yeyote atakayekiuka maadili ya kazi.
Pia alisema amepeleka wahudumu wa afya
wakiwamo wauguzi wawili na daktari mmoja katika zahanati hiyo na huduma
zinaendelea vizuri.
Alipopigiwa simu jana ili azungumzie
uamuzi huo, daktari huyo alianza kumlaumu mwandishi aliyeandika habari ya tukio
hilo akisema kuwa amemharibia kazi.
“Sikutegemea kama wewe uko hivyo, sasa
nimekujua kumbe uko hivyo, Mungu mkubwa, yaani mmepigiwa simu na watu na kuamua
kuja kuniharibia,” alisema Dk Msafiri na kukata simu kisha akaandika ujumbe
uliosema: “Sikukujua sasa nimekujua vizuri, Mungu mkubwa.
Post a Comment