Wananchi wa kijiji cha Chogo kata ya mapanda wilayani mufindi mkoani Iringa wamelalamikia kuhusu kuny”ang”anywa kinguvu ardhi yao zaidi ya  hekari 500 ambazo ni mali ya kijiji hicho.
 
Wakizungumza na waandishi wa habari kijijini hapo wananchi hao wamedai kuwa wamenyang”anywa ardhi hiyo na bwana Godfrey Mosha ambaye pia ni  mjumbe wa NEC mkoa wa iRinga kupitia chama cha mapinduzi ccm.
 
Aidha wananchi hao wamedai kuwa Bwana Mosha amekuwa  akiwafanyia vitendo vya kinyama baadhi ya wananchi anaowakuta wakifanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo ndani ya shamba hilo ambapo wamedai amekuwa akiwatishia kwa bunduki mara kadhaa na kuwapiga huku akiwa amewavua nguo jambo ambalo wanaona ni kunyanyaswa na kuwadhalilisha katika ardhi yao wenyewe.
 
Hivi majuzi baadhi ya wananchi wakiwa katika shughuli za upandaji miti ndani ya shamba hilo mara akatokea bwana mosha akiwa na mfanyakazi wake na kuanza kuwapiga na kuwatishia na bunduki ikiwa na risasi za moto kutokana na kuchoshwa na unyanyasaji wa mara kwa mara unaofanywa na kibosile huyo  wakaamua kujitoa muhanga na kumnyang”anya silaha na kuanza kumpa kichapo ambapo baada ya tukio hilo kibosile huyo alichukuliwa na kwenda kutibiwa mkoani Dar es Salaam huku baadhi ya vijana wa kijiji cha Chogo kama ilivyo ada ya yanayotokea huko na nguvu ya fedha na mtandao mkubwa wa viongozi na jeshi la polisi alivyonavyo bwana MOSHA vijana hao walikamatwa na kupelekwa mahabusu.
 
Kwa upande wao wananchi wakiongozwa na Mtendaji na mwenyekiti wa kijiji cha Chogo wamedai kuchoshwa na hali hiii ambapo wanadai kuwa wamekwishatoa taarifa kwa mkuu wa mkoa wa  Iringa ambaye amedai kuwasaidia huku mkuu wa wilaya ya Mufindi Bi evarista kalalu akidai kuwa hawezi kumwajibisha kada huyo wa CCM na kuwataka wananchi kusubiri hadi utakapomalizika uchaguzi wa mwaka 2015 ndipo alishughulikie jambo hilo.
 
Pia wananchi hao wanadai Mosha amekuwa akijigamba kuwa jeshi la polisi, viongozi wa chama na serikali ni watu anaowamudu hivyo hakuna anayeweza kumfanya jambo lolote hatua ambayo wananchi wanadai anayafanya haya kwa kuwa ni kiongozi wa chama tawala na mkewe ni mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi taifa na wao wamedai kuwa wamesikia tetesi za mkewe kutaka kuwania ubunge katika jimbo la mufindi kusini ambapo wamesema watapita katika kila kata kuwaomba wananchi hao wa mufindi kusini kutomchagua katika nafasi hiyo.

Post a Comment

 
Top