Mfanyabiashara mmoja mwanamke mjini Njombe ameshangazwa kuona kuku wake hawatagi kwa muda mrefu wakati jogoo aliyemnunua alikuwepo lakini alichokigundua ni kuwa jogoo huyo hakuwa na uwezo wa kumpanda tetea.

Mwana mama huyo aliamua kumchinja na kumfanya kitoweo chakushangaza ni pale alipo mpasua ndani yake na kubaini kuwa hakuwa na mayai.

Kwa mujibu wa madaktari wa mogonjwa ya uzazi kutoka kitengo cha uzazi katika hospitali ya rufaa jijini Mbeya Dokta Makulila baada ya kuzungumza na Kings radio amesema hajawahi kusikia kitu kama hicho kwa wanyama lakini kwa binadamu ni kawaida sana kutokea.

Kwa mujibu wa daktari wa mifugo na mtafiti kutoka mkoani Njombe kusini mwa Tanzania  Harrison Gabriel amesema kitaalamu inawezekana na tatizo hilo kisayansi linaitwa Infertility na kitu ambacho jagoo anazaliwa nacho.

Kuhusu kupatikana kwa tiba Harrison amesema  hilo ni Genetical prolem kwa kiingereza na liko nje nje ya uwezo wa wataamu kwani tatizo ambalo jogoo anazaliwa nalo.

Post a Comment

 
Top