Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameteuliwa kuwa rais bora barani Afrika katika mwaka 2014-2015. 

Chama cha Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Barani Afrika (AASU) kimemtunuku Rais Kenyatta tuzo hiyo kutokana na juhudi zake za kuboresha sekta ya elimu na kuimarisha hali ya maisha ya wananchi wa kawaida.

 Akipokea tuzo hiyo jijini Nairobi mapema leo, Rais Kenyatta amesema atajitahidi kuona elimu ya juu katika taasisi za serikali nchini Kenya inapatikana bila malipo katika siku za usoni. 

Rais wa Kenya amewataka wanafunzi wa elimu ya juu barani Afrika kuwa na mazoea ya kufanya mazungumzo na viongozi wao kila mara panapotokea matatizo ili kuepusha visa vya wanafunzi wa vyuo vikuu kufanya migomo ambayo huandamana na fujo. 

Mwaka uliopita, Rais Paul Kagame wa Rwanda ndiye aliyetunukiwa tuzo hiyo ya kuwa rais bora zaidi barani Afrika katika mwaka 2013-2014.

Post a Comment

 
Top