Naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania bara Rajab Luhavi.
 Hatiamaye zoezi la kuchukua na kurudisha fomu kwa makada wa chama cha mapinduzi ccm wanaowania kuchaguliwa kugombea urais limemalizika ambapo makada 38 wamerudisha fomu baada ya kutimiza masharti ya kutafuta wadhamini, huku makada wengine wanne wakishindwa kurudisha fomu hizo ndani ya muda uliopangwa.

Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania bara Rajab Luhavi amesema mchakato huo umeenda vizuri kulingana na utaratibu ulivyopangwa huku idadi kamili ya waliochukua fomu hizo wakiwa ni 42 na waliorudisha ni 38.

Amewataja walioshindwa kurudisha fomu kuwa ni Peter Isaya Nyalali, Dkt Muzamili Musa Kalokola, Mwalimu Antony Khalfan Chalamila na Hellena Alinawinga ambaye aliziacha fomu zake palepale makao makuu mara baada ya kuzichukua.

Miongoni mwa makada waliohitimisha zoezi hilo leo ni naibu waziri wa mawasiliano sayansi na teknolojia January Makamba ambaye ameonya mchakato wa uchaguzi usitumike kuharibu amani iliyopo nchini huku akiwataka wana CCM kuhakikisha wanachagua mgombea anayekijua chama vizuri .

Kada mwingine aliyerudisha fomu ni Wiliam Nngeleja mbunge wa Sengerema ambaye pamoja na mambo mengine amesema endapo atapata ridhaa ya wana CCM atahakikisha anawekeza kwenye makundi makubwa yaliyopo ndani ya jamii ambayo ni wakulima wafanyakazi wavuvi na wafugaji ili kuondoka na uchumi tegemezi na kupiga hatua katika maendeleo .

Post a Comment

 
Top