Vikundi vya wajasiliamli vilivyopo wilyani Mufindi mkoani iringa vimeungana na kuunda umoja wa vikundi hivyo UVIKIMU na kujipanga kushirikiana katika uzalishaji mali na kuinuana kiuchumi.

Uzinduzi wa umoja huo umefanyika mapema tar.05, April 2014 katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi mjini Mafinga na kuhudhuriwa na wanachama wa vikundi zaidi ya 5 huku wakiungwa mkono na mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarista kalalu.

Lakini licha ya vikundi hivyo kuunda umoja huo na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijasrliamali ikiwemo ufugaji wa kuku, uoteshaji wa miti na kilimo cha kisasa, changamoto kubwa inayowakabili wajasiriamali hao ni kukosa suport kutoka serikalini na taasisi zingine kwa kuto waunga mkono kwa kununua bidhaa zao.

Kwa upande wa uzalishaji miti, mwitikio umekuwa mkubwa lakini baada ya miti kuoteshwa imekuwa ikikosa wateja kwa muda mrefu na kupelekea miti hiyo kuharibika na kukauka kutokana na kupita kwa umri wa kuendelea kukaa vitaloni.

Akizungumza na mwanahabari mwenyekiti wa umoja wa vikundi vya kimaendeleo Mufindi UVIKIMU Osca Kikungwe ameeleza hatua za uoteshaji wa miti hiyo hadi kufikia hatua ya kuuzwa kuwa inafikia gharama ya zaidi ya sh. mil. 9 kwa miche 30,000, jambo linalowapelekea wakulima kukata tamaa.

Mwenyekiti huyo ametoa wito kwa serikali na kuitaka badala ya kwenda kununua miti kwenye taasisi nakwingineko ni vema ikafika katika mashamba ya wajasiriamali hao ikiwezekana itoe na elimu juu ya uzalishaji bora wa mbegu na uoteshaji.


                               Miche ya miparachichi iliyooteshwa katika moja ya vitalu
                               na kukosa wanunuzi.
Miche ya miti ya mbao aina ya SYPRUS iliyokwisha kukaa kwa muda mrefu 
kwenye kitalu na sasa mbioni kuharibika.
                                Wanachama wa UVIKIMU wakiwa katika vitalu vya miti
                                iliyozalishwa na mwanachama mwenzao katika kata ya Boma mjini Mafinga
                                Wilayani Mufindi.
                                            Mmoja kati ya wajasiliamali akiwa katika katika
                                            shamaba lake ambaye anadai kuwa endapo miti
                                            hiyo haita nunuliwa kwa muda wa miezi miwili
                                            mbele atakuwa ameingia hasara ya zaidi ya milioni
                                            9.

Next
Newer Post
Previous
This is the last post.

Post a Comment

 
Top