Wajumbe wa kimataifa wanakutana
katika kongamano mjini Oslo Norway, kuchanga fedha za kuisaidia Sudan Kusini
inayokumbwa na mapigano kwa takriban miezi minne sasa.
Umoja wa mataifa unasema dola
bilioni 1.26, zinahitajika kuwasaidia mamilioni ya watu katika taifa hilo
changa Afrika, wanaokabiliwa na njaa.
Kwa mujibu wa Umoja huo, takriban
raia milioni saba wa nchi hiyo huenda wakahitaji usaidizi wa kibinadamu.
Hali imezidi kuwa nzito kutokana na
uwezekano wa kuwadia kwa msimu wa mvua utakaosababisha kutoweza kutumika kwa
barabara chache zilizopo, na maeneo ya kututa ndege.
Hilo litatatiza usafirishaji wa
misaada katika maeneo mengi nchini humo.
Radio Tehran.
Post a Comment