Umati wa watu pamoja na jeshi lazimamoto katika mji wa Jos wakijaribu kuuzima moto uliosambaratisha majengo pamoja na magari katika eneo hilo.
Jeshi la serikali ya Nigeria kwa kushirikiana na madaktari wakipakia miili ya watu waliouawa katika shambulio hilo.
Maafisa nchini Nigeria wamesema kuwa wamepata maiti 118 kufuatia shambulio la bomu katika mji wa Jos.
Dakika 20 baadaye mlipuko wa pili ulitokea karibu na hospitali.
Inahofiwa kuwa kuna maiti zaidi zilizonaswa kwenye vifusi vya majengo yaliyo poromoka kutokana na shambulio hilo.
Kufikia sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo lakini wengi wanaamini kuwa Kundi la wapiganaji wa kiislamu la Boko Haram lilihusika.
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amejitokeza kukemea mashambulio hayo na kusema kuwa amejitolea kuangamiza kabisa ugaidi.
Post a Comment