Huyu ndiye mbwa aliyefanya wananchi wa Ludewa mjini waandamane hadi kwa mmiliki na kumuua akiwa bandani baada ya kumla mtoto wa darasa la tatu.
 Mbwa aliyeuawa awali katika eneo ambalo mtoto aliliwa.
Jeneza lililobeba mwili wa mtoto Ibrahim ambaye aliuawa na Mbwa.

Mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina la Ibrahim Faraja Chipungahelo(9) aliyeishi mtaa wa Ibani wilayani Ludewa katika mkoani Njombe ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Kimbila mwishoni mwa wiki iliyopita alivamiwa na Mbwa kisha kutafunwa hadi kufa papo hapo wakati akijitahidi kuwaokoa watoto wenzake ambao walizongwa na mbwa hao wawili.
Shuhuda aliyekuwa katika tukio hilo Mama haule akisimulia mkasa huo alisema watoto hao walikuwa atano ambapo marehemu na wenzake walikua wakienda nyumbani kwa babu yao kuchuma matunda aina ya mapera na kukutwa na mkasa huo.
Mama Haule alisema Marehemu Ibrahimu na watoto wenzie ilikuwa ni kawaida yao kupita katika maeneo ya Ikulu ya wilaya ya Ludewa wakielekea kwa babu yao lakini eneo hilo la Ikulu limekuwa hatari kutokana na mwananchi mmoja ambaye ni Bosco Lingalangala kununua nyumba moja ambayo amefuga mbwa wawili wakali wasio kuwa na uangalizi wakutosha.

Post a Comment

 
Top